Karibuni Vijana na Wadau mbalimbali wapenda maendeleo ya Kigamboni yetu pendwa... Ndani ya Ubalozi wa Vijana Kigamboni (UVIKI)kuna Aina nne (4) za uanachama ambazo ni:
1.Mwanachama muasisi
2.Mwanachama wa kawaida
3.Mwanachama wa heshima
4.Mwanachama mshiriki
Utaona pichani kama zilivyo orodheshwa ndani ya katiba kwa kuna mengi ya kunufaika unapojiunga na Ubalozi wa Vijana Kigamboni.. Kwa ushauri,taarifa,maoni,maswali n.k tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa anuani zetu.. Ahsante
Jumapili, 18 Septemba 2016
Mwenyekiti wa Ubalozi wa Vijana Kigamboni akimkabidhi T-shirt ya chama mkuu mpya wa wilaya wa Kigamboni kama ishara ya kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuleta maendeleo anayoifanya na kumpa ahadi kutoka kwa vijana wa Kigamboni ya kuwa naye bega kwa bega katika kuhakikisha Kigamboni inakua nuru itakayotizamwa duniani koyte 

Ubalozi wa Vijana Kigamboni ulipata bahati ya kuhudhiria kikao kilichoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Kigamboni dhumuni ikiwa ni kukusanya maoni kutoka kwa watu mbalimbali yatakayoweza kusaidia kupandisha ufaulu wa wanafunzi ndani ya wilaya ya Kigamboni.. Kama Ubalozi wa Vijana Kigamboni tunapenda kutoa pongezi za dhati kwa mkuu wetu mpya wa wilaya kwa juhudi zake anazozionyesha katika kuleta maendeleo ya Kigamboni yetu pendwa na wazo lake chanya la kushirikisha jamii inayomzunguka kuweza kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma Kigamboni yetu kimaendeleo
Jumatano, 14 Septemba 2016
Mwenyekiti wa muda bw.#Alfred Tembo akiweka saini yake kwenye katiba ya Ubalozi wa Vijana Kigamboni kama kuthibitisha kuikubaliana nayo... Mambo moto karibuni wadau tujumuike kwa pamoja kuleta fursa kwa vijana ili kuwa komboa kifikra na kiuchumi..

Jumatatu, 12 Septemba 2016
KUZALIWA KWA UVIKI..
Jumapili ya tarehe 11-09-2016 itabaki kua siku ya kukumbukwa na wanaharakati wa maendeleo ya vijana Kigamboni hii ni baaada siku hii mwenyezi mungu kuibariki na kwa uwezo wake UBALOZI WA VIJANA KIGAMBONI(UVIKI) ikazaliwa rasmi.. Ndani ya ukumbi wa Kijiji beach waasisi walikutana na kuweza kupitisha azimio la pamoja la kupitisha katiba itakayoongoza UVIKI kusonga mbele.. Karibuni vijana wa Kigamboni tuungane pamoja maana umoja na mshikamano ndio nguvu yetu









Jumanne, 6 Septemba 2016
KATIBA TOLEO LA KWANZA

Utengenezaji wa katiba
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)