
Katibu tawala wa wilaya ya Kigamboni Ndg Rahel Mhando akifunga semina ya Ujasiriamali kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, aliwaambia washiriki wa semina hiyo kuwa huo ni mwanzo na mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa mara kwa mara ili kuwafanya wajasiliamali wengi kupata Maarifa yatakayowasaidia kuleta tija katika shughuli zao.
DAS Mhando amewahakikishia washiriki wa semina kuwa serikali inachukua
hatua mbalimbali za maksudi ili kuwawezesha wajasiriamali kiuchumi.
Amesema kuwa kupitia balaza la Kuwawezesha wananchi kiuchumi (NEEC)
zipo pesa ambazo hivi karibuni zitaanza kukopeshwa kwa vikundi mbalimbali vya
ujasiliamali katika wilaya ya Kigamboni na hivyo kuwataka waanze kujipanga
katika vikundi.
Aidha, amesema pia kuna pesa itakayotolewa na halmashauri kwa ajili ya
vijana na akina mama, nayo itatolewa katika vikundi, hivyo ni vema
wajasiliamali hao kuwa katika vikundi ili waweze kunufaika na pesa hizo.
Amewahasa washiriki wa semina kuendelea kujihusisha na shughuli zao za
uzalishaji na kujiepusha na vitendo visivyokubalika katika jamii ikiwemo
matumizi ya madawa ya kulevya.
Semina hiyo ilihudhuriwa na vijana na akina mama wapatao 150 kutoka
katika Kata mbalimbali za Wilaya ya Kigamboni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni