Jumapili, 12 Februari 2017

SAFARI ILIPOANZIA,UVIKI KUTOKEA,WATU WALISIKILIZIA,UVIKI KUPOTEA,MUNGU KASIMAMIA,UVIKI KUENDELEA



 SAFARI NI SAFARI INGAWA SI WOTE MTAFIKA MKONO WAKO MUNGU UENDELEE KUSHIKIRIA UVIKI NA WATU WAKE ILI WAWEZE KUFANYA MAPINDUZI YA FIKRA NA UCHUMI KWA JAMII NA VIJANA WA KIGAMBONI.


HISTORIA FUPI YA UBALOZI WA VIJANA KIGAMBONI (UVIKI).

UBALOZI WA VIJANA KIGAMBONI (UVIKI) ni kikundi cha kijamii kilichoanzishwa katika Wilaya ya Kigamboni,Kikundi hiki kilianzishwa ili kuleta mapinduzi ya kifikra na kiuchumi kwa vijana na jamii kwa ujumla pia kurudisha umoja na mshikamano baina ya kijana kwa kijana na kijana kwa jamii ndani ya Kigamboni na nje ya Kigamboni.

ILIPOTOKA
Wazo la kuanzisha umoja huu lilitokana na harakati za kuanzisha chama cha mpira wa miguu Kigamboni katika uwanja wa machava Kigamboni,katika harakati hizo za kuanzisha chama cha mpira kulikuwa na wanaharakti wengi sana wakiwemo,mwalimu bendera,Ramadhani shauritanga,deo lucas,Rashid,Mude,metusela,mecky,Tembo,Thabit na wengine wengi
Hapo ndipo baadhi ya wanaharakati walipo hamua kufanya jambo moja kwa mustakabari wa Kigamboni nzima si kwa michezo tu bali katika Nyanja zote,wanaharakati hao wakiwemo Rashid.A.Rashid,Mecky Michael,Alfred.K.Tembo,Ladislaus.S.Mude,Shilla Hamis,Salum Said,Metusela Obedi,Thabit Molly na Kennedy Gimba.
Kwa pamoja walifanya kikao chao cha kwanza katika uwanja wa machava kikao hicho walikiita KIKAO WIMA (yaani walisimama na kufanya mazungumzo).katika kikao hicho mawazo yalikuja mengi sana na majina mbalimbali juu ya kikundi husika,lakin jina moja tu ndilo lililo kubaliwa na kupitishwa na lilipendekezwa na mwanaharakati Alfred Tembo,jina hilo ni ubalozi wa vijana Kigamboni(Uviki).
Dhumuni kuu lilikuwa sisi tuwe mabalozi na wawakilishi wa vijana wa Kigamboni ndani na nje ya Kigamboni.tukiamini kuwa Kigamboni ina fursa nyingi ambazo vijana wake hawafaidiki nazo.
Ndugu Rashid.A.rashid alilichukua wazo hilo mpaka kwa Ndugu Ramadhani Shauritanga ili kupata njia ya kuanzia ndipo Ndugu Ramadhani kwa kutambua umuhimu wa jambo hili akaamua kutupa muongozo wa katiba wa Chama Cha Vijana Kigamboni (Chaviki),ndugu Ramadhani alikuwa ni katibu wa chama hicho,na alitusihii tuangalie mapungufu ambayo yaliwafanya wao kushindwa kuendelea na umoja wao huo.
Tulianza vikao mara moja katika chumba cha Ndugu Rashid.A.Rashid kwa kuichambua katiba hile ya Chaviki  na kuangalia mapungufu yao,hakika safari ilikuwa ngumu na yenye changamoto nyingi zikiwemo za muda,pesa na wengine kuishia njia kutokana na ugumu uliyopo.
Hakika Mungu alitusimamia ipasavyo kwa kuwa alijua kuwa tuna nia ya kweli ya kuifikisha Kigamboni sehemu inayostaili kufika.
Tulionelea hatuwezi kuendesha chama au kuandaa katiba tukiwa na jinsia moja ndipo tulipo kubaliana na kufanya maamuzi ya kuunganisha nguvu na mawazo na jinsia nyingine, ndipo walipo kuja wanaharakati wa kike,Salome John,Sakina Athumani,Jesca  Na Farida.J.Mtoto na kutimia timu ya watu kumi na tatu.
Kwa umoja wetu tulipambana vya kutosha kufanikisha kuipata katiba ya UVIKI, OFISI YA UVIKI, WALEZI NA WADHAMINI,bila kuwasahau WANACHAMA WA UVIKI,pia tukiwa tunaendelea na mchakato wa USAJILI na sasa upo katika ngazi ya kitaifa tushamaliza ngazi ya wilaya.
Tulianza wengi na wengine kuishia njian kutokana na changamoto mbalimbali za kijamii.
Bodi ya waasisi wa ubalozi wa vijana Kigamboni inawashukuru wote waliochangia kwa kiasi kikubwa kuisaidia kwa kipindi chote kigumu cha mchakato wa kuusimamisha umoja huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni