Jumanne, 21 Februari 2017

WAJASIRIAMALI KIGAMBONI KUNUFAIKA NA MIKOPO.







Katibu tawala wa wilaya ya Kigamboni Ndg Rahel Mhando akifunga semina ya Ujasiriamali kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, aliwaambia washiriki wa semina hiyo kuwa huo ni mwanzo na mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa mara kwa mara ili kuwafanya wajasiliamali wengi kupata Maarifa yatakayowasaidia kuleta tija katika shughuli zao.

DAS Mhando amewahakikishia washiriki wa semina kuwa serikali inachukua hatua mbalimbali za maksudi ili kuwawezesha wajasiriamali kiuchumi.

Amesema kuwa kupitia balaza la Kuwawezesha wananchi kiuchumi (NEEC) zipo pesa ambazo hivi karibuni zitaanza kukopeshwa kwa vikundi mbalimbali vya ujasiliamali katika wilaya ya Kigamboni na hivyo kuwataka waanze kujipanga katika vikundi.

Aidha, amesema pia kuna pesa itakayotolewa na halmashauri kwa ajili ya vijana na akina mama, nayo itatolewa katika vikundi, hivyo ni vema wajasiliamali hao kuwa katika vikundi ili waweze kunufaika na pesa hizo.

Amewahasa washiriki wa semina kuendelea kujihusisha na shughuli zao za uzalishaji na kujiepusha na vitendo visivyokubalika katika jamii ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.

Semina hiyo ilihudhuriwa na vijana na akina mama wapatao 150 kutoka katika Kata mbalimbali za Wilaya ya Kigamboni.

UPENDO,UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO NGUZO YA UVIKI


UPENDO,UMOJA NA MSHIKAMANO WA UVIKI UMETOKANA NA VIUNGO VYA MWILI WA MWANADAMU.AMINI NAWAAMBIA KILA KIUNGO CHA MWANA KINAPENDANA NA MWENZIE NDIO MAANA NI WAMOJA PIA USHIRIKIANA.
KIDOLE KIKIUMA BASI KICHWA KITAWAZA KWA MAUMIVU,MDOMO UTASONONEKA.
TUMBO LIKIUMA BASI MKONO UTAENDA KUMSHIKA ILI KUMFARIJI.

UVIKI TUPO PAMOJA NA LENGO NI KUKUINUA WEWE KIJANA,ILI UWEZE KUJITAMBUA NA KUUJUA UMUHIMU WAKO KATIKA JAMII YAKO NA TAIFA KWA UJUMLA.






KIJANA AMKA CHANGAMKIA FURSA(SEMINA YA UJASIRIAMALI

UVIKI NI KIKUNDI CHA KIJAMII KILICHOANZISHWA NA VIJANA WANAHARAKATI WA KIGAMBONI KWA DHUMUNI LA KULETA MAPINDUZI YA KIFIKRA NA KIUCHUMI KWA VIJANA NA JAMII YA KIGAMBONI.
SEMINA YA VIJANA KUHUSU UJASIRIAMALI NI MOJA YA MALENGO YA UVIKI TUNA SHUKURU OFISI YA MKUU WA WILAYA WAKISHIRIKIANA NA TYVA KULETA SEMINA HII KWA VIJANA WA KIGAMBONI.

UVIKI TUNA AMINI KUWA "KUJIARI NI BAHARI NA KUAJIRIWA NI GEREZA"
NAJUA WATAKUJUA NINI MAANA HALISI YA MANENO HAYA TEGA SIO NA FUATILIA KWA UKARIBU HARAKATI ZA UVIKI UTAPATA MAJIBU YA MANENO HAYO.

UPENDO,UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO NGUZO YETU KUU


 SHUKRANI KWAKO DADA REHEMA KHALIFA


SEMINA YA VIJANA KUHUSU UJASIRIAMALI

 WANA UVIKI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KIGAMBONI MHE. RAHEL A.MUHANDO KATIKA SEMINA YA VIJANA KUHUSU UJASIRIAMALI ILIYO FANYIKA KATIKA UKUMBI WA CCM-KIGAMBONI
 WANAUVIKI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KATIBU WA MKUU WA WILAYA NDUGU PIUS MPWEZA


Jumapili, 12 Februari 2017

UVIKI MEMBERS


 BODI YA WAASISI WAKIWA NA MHE.DOTTO MSAWA,MHE.SANYA BUNAYA NA MLEZI NDUGU RAMADHAN SHAURITANGA,

 WANACHAMA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MHE.DOTTO MSAWA,MHE.SANYA BUNAYA NA MLEZI
 HAKIKA HAIKUWA RAHISI NA HAITAKUWA RAHISI
 JASHO LAKO,UKOMBOZI WETU
 UVIKI KIGAMBONI INA TUMAINI NAWE
KUCHOKA KWAKO NI MATAABIKO KWETU.




UVIKI TUNAKUOMBEA UZIDI KUSONGA MBELE,WEWE NDIO KIJITO CHETU CHA MATUMAINI.

SAFARI ILIPOANZIA,UVIKI KUTOKEA,WATU WALISIKILIZIA,UVIKI KUPOTEA,MUNGU KASIMAMIA,UVIKI KUENDELEA



 SAFARI NI SAFARI INGAWA SI WOTE MTAFIKA MKONO WAKO MUNGU UENDELEE KUSHIKIRIA UVIKI NA WATU WAKE ILI WAWEZE KUFANYA MAPINDUZI YA FIKRA NA UCHUMI KWA JAMII NA VIJANA WA KIGAMBONI.


HISTORIA FUPI YA UBALOZI WA VIJANA KIGAMBONI (UVIKI).

UBALOZI WA VIJANA KIGAMBONI (UVIKI) ni kikundi cha kijamii kilichoanzishwa katika Wilaya ya Kigamboni,Kikundi hiki kilianzishwa ili kuleta mapinduzi ya kifikra na kiuchumi kwa vijana na jamii kwa ujumla pia kurudisha umoja na mshikamano baina ya kijana kwa kijana na kijana kwa jamii ndani ya Kigamboni na nje ya Kigamboni.

ILIPOTOKA
Wazo la kuanzisha umoja huu lilitokana na harakati za kuanzisha chama cha mpira wa miguu Kigamboni katika uwanja wa machava Kigamboni,katika harakati hizo za kuanzisha chama cha mpira kulikuwa na wanaharakti wengi sana wakiwemo,mwalimu bendera,Ramadhani shauritanga,deo lucas,Rashid,Mude,metusela,mecky,Tembo,Thabit na wengine wengi
Hapo ndipo baadhi ya wanaharakati walipo hamua kufanya jambo moja kwa mustakabari wa Kigamboni nzima si kwa michezo tu bali katika Nyanja zote,wanaharakati hao wakiwemo Rashid.A.Rashid,Mecky Michael,Alfred.K.Tembo,Ladislaus.S.Mude,Shilla Hamis,Salum Said,Metusela Obedi,Thabit Molly na Kennedy Gimba.
Kwa pamoja walifanya kikao chao cha kwanza katika uwanja wa machava kikao hicho walikiita KIKAO WIMA (yaani walisimama na kufanya mazungumzo).katika kikao hicho mawazo yalikuja mengi sana na majina mbalimbali juu ya kikundi husika,lakin jina moja tu ndilo lililo kubaliwa na kupitishwa na lilipendekezwa na mwanaharakati Alfred Tembo,jina hilo ni ubalozi wa vijana Kigamboni(Uviki).
Dhumuni kuu lilikuwa sisi tuwe mabalozi na wawakilishi wa vijana wa Kigamboni ndani na nje ya Kigamboni.tukiamini kuwa Kigamboni ina fursa nyingi ambazo vijana wake hawafaidiki nazo.
Ndugu Rashid.A.rashid alilichukua wazo hilo mpaka kwa Ndugu Ramadhani Shauritanga ili kupata njia ya kuanzia ndipo Ndugu Ramadhani kwa kutambua umuhimu wa jambo hili akaamua kutupa muongozo wa katiba wa Chama Cha Vijana Kigamboni (Chaviki),ndugu Ramadhani alikuwa ni katibu wa chama hicho,na alitusihii tuangalie mapungufu ambayo yaliwafanya wao kushindwa kuendelea na umoja wao huo.
Tulianza vikao mara moja katika chumba cha Ndugu Rashid.A.Rashid kwa kuichambua katiba hile ya Chaviki  na kuangalia mapungufu yao,hakika safari ilikuwa ngumu na yenye changamoto nyingi zikiwemo za muda,pesa na wengine kuishia njia kutokana na ugumu uliyopo.
Hakika Mungu alitusimamia ipasavyo kwa kuwa alijua kuwa tuna nia ya kweli ya kuifikisha Kigamboni sehemu inayostaili kufika.
Tulionelea hatuwezi kuendesha chama au kuandaa katiba tukiwa na jinsia moja ndipo tulipo kubaliana na kufanya maamuzi ya kuunganisha nguvu na mawazo na jinsia nyingine, ndipo walipo kuja wanaharakati wa kike,Salome John,Sakina Athumani,Jesca  Na Farida.J.Mtoto na kutimia timu ya watu kumi na tatu.
Kwa umoja wetu tulipambana vya kutosha kufanikisha kuipata katiba ya UVIKI, OFISI YA UVIKI, WALEZI NA WADHAMINI,bila kuwasahau WANACHAMA WA UVIKI,pia tukiwa tunaendelea na mchakato wa USAJILI na sasa upo katika ngazi ya kitaifa tushamaliza ngazi ya wilaya.
Tulianza wengi na wengine kuishia njian kutokana na changamoto mbalimbali za kijamii.
Bodi ya waasisi wa ubalozi wa vijana Kigamboni inawashukuru wote waliochangia kwa kiasi kikubwa kuisaidia kwa kipindi chote kigumu cha mchakato wa kuusimamisha umoja huu.

FURSA SIO KUPEWA PESA AU MRADI KUWA KARIBU NA VIONGOZI NI FURSA YA KIPEKEE

 MHE.DOTTO MSAWA WA JUU  NA MHE.SANYA BUNAYA CHINI WAKITOA NASAHA KWA VIJANA WA UVIKI KATIKA MKUTANO WA KWANZA WA UVIKI MIAMI  TRH 11/02/2017.


NA IKUMBUKWE HII SIKU